UTUME KWA VIJANA 9
Sahaya G. Selvam, SDB
“Tumekuja Kumwabudu”
Siku ya Vijana Duniani na Utume Kwa Vijana
Tarehe 16 hadi 21, mwezi Agosti, mwaka 2005 vijana wapatao millioni moja wanatarajiwa kukutanika huko Koloni nchini Ujerumani. Kongamano hili limekuwa maarufu sana na linajulikana kwa jina la “Siku ya Vijana Duniani” – World Youth Day. Siku ya Vijana Duniani (SVD) huadhimishwa kila mwaka katika majimbo ya Kanisa Katoliki siku ya Jumapili ya Matawi. Lakini mara kwa mara huadhimishwa kimataifa, kwa muda wa wiki moja, kama hii ya mwaka huu huko Koloni. Kwa kawaida, kabla ya wiki ya kongamano lenyewe vijana hukaribishwa katika majimbo mbalimbali ya nchi husika. Wiki kabla ya SVD katika majimbo inawapa vijana wageni nafasi ya kushiriki katika maisha ya vijana wenyeji, na kubadilishana mawazo kuhusu matatizo ya dunia na hali ya Kanisa. Wiki ya “World Youth Day” yenyewe ina vipindi vya Katekesi, nafasi za sala, na hija; wiki ya kongamano hufungwa kwa […]
Youth ministry
Lectio Divina
UTUME KWA VIJANA 12
Sahaya G. Selvam, SDB
Lectio Divina Kwa Vijana
Tangu mwaka 1985, imekuwa desturi katika Kanisa Katoliki kuadhimisha Jumapili ya Matawi kuwa Siku ya Vijana Duniani. Aidha, kila mwaka katika adhimisho hili Baba Mtakatifu huwa anatoa ujumbe maalumu kwa ajili ya vijana duniani kote. Hata mwaka huu wa 2006, katika adhimisho la 21 la Siku ya Vijana Duniani (9 April 2006), Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kwa vijana wote: “Dhamira ninayopendekeza kwenu ni kutoka Zaburi 119: 105 – “Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.”
Katika ujumbe wake anasisitizia kuwa vijana wa siku hizi tunaishi katika mazingira magumu yenye falsafa za uongo na maadili potofu. Katika mazingira haya ya giza Neno la Mungu ndilo linaloweza kuiangaza njia yetu.
Papa anatukumbushia maneno ya mwandishi wa Waraka kwa Waebrania anayesema: “Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo […]
Vijana na Tabia hatari
UTUME KWA VIJANA 13
Sahaya G. Selvam, SDB
Sababu za Vijana Kujingiza katika Tabia za Hatari
na Namna ya Kuwasaidia
Katika makala hii tunashirikisha namna ya kuwasaidia vijana ili waweze kuvuka vikwazo vinavyoweza kuwafanya wasifikie malengo waliojiwekea maishani mwao. Tunatambua kwamba, yapo mambo mengi yanayoweza kuwachelewesha au kuwakwaza vijana kutofikia malengo yao ya maisha. Baadhi yake ni kama:
Dawa za kulevya
Ulevi
VVU/Ukimwi
Mimba kabla ya wakati, n.k.
Katika makala hii, tunaelezea sababu chache zinazopelekea vijana (wasichana) kupata mimba kabla ya wakati. Pia tunapendekeza namna ya kuweza kuwasaidia ili wasijikute katika mtego huu na pia waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Ingawa sababu hizi zinawalenga wasichana moja kwa moja, hata hivyo zinaweza kutumika kwa wavulana pia, kwa vile wavulana wanajiingiza katika mambo haya kirahisi kuliko wasichana.
Bi. Tricia M. Davis amefanya utafiti kati ya wasichana wapatao 500 wenye umri wa miaka chini ya 19, waliowahi kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika utafiti wake anaeleza sababu saba […]