UTUME KWA VIJANA 6
Sahaya G. Selvam, SDB
Vyama Mbalimbali na Malezi ya Vijana
Kuwapenda watu, na kupendwa na watu ni mojawapo ya mahitaji ya kila binadamu. Hitaji hili linaamshwa wakati wa ujana. Hali hii hutokana na mabadiliko ya kimaumbile, kihisia na ya kiakili yanayotokea wakati wa ujana. Ndiyo maana vijana huwa wanahangaika sana na suala la kutafuta marafiki na namna ya kukuza mahusiano na watu, hasa uhusiano na watu wa jinsia tofauti.
Malezi ya jumla kwa vijana yanapaswa kuwapa vijana nafasi ya kukomaa kihisia na kijamii. Ukomavu huu unaweza kukamilishwa kwa njia ya vikundi na vyama vya vijana. Hakuna anayeweza kujifunza namna ya kujenga mahusiano yanayofaa isipokuwa kwa njia ya kupata nafasi ya kuwa katika mazingira ya kuzoeana na watu. Kazi ya vyama vya vijana ni kuwatengenezea vijana mazingira haya. Vijana wenyewe wanapenda sana kujiunga na vikundi mbalimbali na kushiriki katika shughuli za vikundi kwa sababu ya hitaji lao la kupenda na […]