UTUME KWA VIJANA 8
Sahaya G. Selvam, SDB
Vijana na Vyombo vya Mawasiliano
Tupende tusipende nyakati hizi za karne ya 21 tumelazimika kutumia vyombo mbalimbali vya mawasiliano, kama vile, magazeti, simu, redio, kinasa sauti, runinga, video, mtandao, n.k. Vyombo hivi vimechangia katika kufanyia dunia yetu kuwa ndogo sana. Vinachangia katika kuendeleza utandawazi, na katika usambazaji wa utamaduni wa kimagharibi. Tunaweza kuvitumia vyombo hivi kwa ajili ya kujielimisha na kujiburudisha. Maendeleo ya vyombo hivi yanatubabaisha. Yaani, kila wakati vyombo hivi vinakuwa vya teknolojia mpya na vya rahisi kutumia.
Kwa vile, ni kawaida kwa vijana kuvutiwa na mambo mapya, hata maendeleo ya vyombo vya mawasiliano yanawashangaza sana. Vijana wanapenda pia kuunganika daima na vijana wenzao kwa njia ya kuvitumia vyombo hivi. Kwa hiyo, wao huwa wanapenda kuzitumia aina mpya za vyombo vya mawasiliano, na pia kuvitumia sana.
Dunia ya mawasiliano inaweza kuchochea ubunifu wa vijana. Inaweza kuwasaidia kujielimisha na kujiburudisha. Aidha, inaweza kusababisha vijana kupoteza mali na […]