UTUME KWA VIJANA 3
Sahaya G. Selvam, SDB
Malezi jumla kwa Vijana
Naye Yesu Akakua…
Mtoto Yesu alipoanza kuingia katika ujana wake, akiwa na umri wa miaka kumi na miwili, alianza kutafuta maana ya maisha yake. Alitaka uhuru zaidi kutimiza malengo ya maisha yake. Ndiyo maana alikuwa amepotea hekaluni. Alianza kutambua kwamba ilikuwa inampasa kuwa katika nyumba ya Baba yake! Lakini mwinjili Luka anatuambia kwamba baada ya wazazi wake kumwona,
“Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii…. Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima, na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.” (Lk 2:51-52)
Nafsi ya kila binadamu ina vipengele vinne. Hivi ni Mwili, Akili, Hisia (Moyo) na Roho. Vipengele hivi vinaendana na mahitaji manne makuu ya binadamu. Sisi binadamu tunataka kuishi; tunatafuta usalama na raha ya kimwili. Ya pili, tunataka kujifunza mambo mapya, yaani kukuza akili zetu. Ya tatu, daima binadamu hutafuta uhusiano na watu; tunataka kuwapenda watu na kupendwa na watu; ndiyo haya mahitaji […]