UTUME KWA VIJANA 4
Sahaya G. Selvam, SDB
Namna ya Kuwafundishia Vijana ili
Kuleta Mabadiliko ya Tabia
“Semina, semina, semina! Nimechoka na semina hizi!”, kijana mmoja alinilalamikia mara baada ya kurudi kutoka Kongamano la Pasaka.
Nilikuwa ninaongea na Askofu wa jimbo moja la Tanzania, na nikamwambia, “Baba askofu, nimesikia kwamba asilimia kubwa ya vijana wa mkoa huu wameathirika na ukimwi, kama kanisa tumefanya nini kukabiliana na hali hii?” Akanijibu mara moja kwa uhakika, “Tumefanya semina nyingi tu!”
Semina, semina, semina! Je, semina hizi huleta mabadiliko ya tabia? Au semina hizi ni njia mojawapo ya kula misaada tunayoipata kutoka nchi za nje badala ya kukabiliana na matatizo ya kijamii kama ukimwi?
Hakika, zipo njia nyingi tu za kutoa malezi kwa vijana, baadhi zake nimekwisha kuzitaja katika toleo lililopita. Licha ya michezo na vitendo mbalimbali katika vikundi, njia kubwa ya kutoa malezi kwa vijana ni kwa njia ya mafundisho darasani, semina na warsha. Katika makala hii, ningependa […]