Katekisimu kwa ajili ya Vijana – 2

UTUME KWA VIJANA – 17
Sahaya G. Selvam, SDB
Katekisimu kwa ajili ya Vijana – 2
Utangulizi:
Katika makala iliyopita tulieleza malengo ya “Katekisimu hii kwa ajili ya Vijana” na tulitoa maswali 11 pamoja na majibu yake.  Katika makala hii tunaendelea na mfulilizo huo.
 
12. Kwa nini niungame kwa padre?
Ninapotenda dhambi ninajitenga na Mungu na kanisa (yaani Jumuiya/jamii).  Padre kama mwakilishi wa Mungu na kanisa ananipatanisha na Mungu na kanisa.  Pili, Mungu asiyeonekana ananijulisha kuwa amenisamehe kwa njia ya vitendo na maneno katika nafsi ya padre anayeonekana.
 
13. Katika sakramenti ya maungamo nieleze dhambi namna gani?
Ili nipate uponyaji kwa dhambi zangu, niwe nataja tendo nililofanya pamoja na mazingira na lengo lililokuwa nalo nilipotenda dhambi, kama nikiona linaweza kuathiri uzito wa dhambi.
 
Kwa kweli nikiwa nataja dhambi za jumla (k.m. nilivunja amri ya sita), hivi sitaonja uponyaji mwenyewe.  Ninapoeleza wazi dhambi zangu ninaonyesha pia moyo wa majuto pamoja na nia ya kujirekebisha, kwa neema ya Mungu.
 
14. Mbona sisi […]

Continue reading