UTUME KWA VIJANA 13
Sahaya G. Selvam, SDB
Sababu za Vijana Kujingiza katika Tabia za Hatari
na Namna ya Kuwasaidia
Katika makala hii tunashirikisha namna ya kuwasaidia vijana ili waweze kuvuka vikwazo vinavyoweza kuwafanya wasifikie malengo waliojiwekea maishani mwao. Tunatambua kwamba, yapo mambo mengi yanayoweza kuwachelewesha au kuwakwaza vijana kutofikia malengo yao ya maisha. Baadhi yake ni kama:
Dawa za kulevya
Ulevi
VVU/Ukimwi
Mimba kabla ya wakati, n.k.
Katika makala hii, tunaelezea sababu chache zinazopelekea vijana (wasichana) kupata mimba kabla ya wakati. Pia tunapendekeza namna ya kuweza kuwasaidia ili wasijikute katika mtego huu na pia waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Ingawa sababu hizi zinawalenga wasichana moja kwa moja, hata hivyo zinaweza kutumika kwa wavulana pia, kwa vile wavulana wanajiingiza katika mambo haya kirahisi kuliko wasichana.
Bi. Tricia M. Davis amefanya utafiti kati ya wasichana wapatao 500 wenye umri wa miaka chini ya 19, waliowahi kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika utafiti wake anaeleza sababu saba […]