Maisha ya Kiroho – 1

UTUME KWA VIJANA 10
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Vijana, Tunaitwa kuwa Watakatifu!
Maisha ya Kiroho Kwa Vijana – 1
 
Sote Tumeitwa kuwa Watakatifu
 
Mtaguso wa pili wa Vatikano ulitukumbusha kuwa sisi sote tumeitwa kuwa watakatifu:  “Bwana Yesu, aliye Mwalimu na mfano wa kimungu wa kila ukamilifu, aliwahubiria wafuasi wake, wote na kila mmoja wa kila cheo na hali, utakatifu wa maisha, ambao Yeye huwa mtungaji na mtimilizaji wake. ‘Muwe wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu’ (Mt. 5:48).” (Hati ya Mwanga wa Mataifa, na. 40)
 
Kila mmoja katika maisha yake ya kila siku, anatafsiri agizo hili la Yesu kadiri ya nafasi yake na tena kulingana na wito wake – kama mlei, mtawa au padre.   Ingawa kila mmoja anaishi maisha yake kwa namna tofauti, wito wa kuwa mtakatifu ni mmoja.  Katika miaka iliyofuata Mtaguso wa pili wa Vatikano kanisa limeonesha wazi kwamba kuwa utakatifu si jambo la zamani, wala si nafasi pekee kwa wamonaki tu.  Kudhihirisha […]

Continue reading


Maisha ya Kiroho – 2

UTUME KWA VIJANA 11
Sahaya G. Selvam, SDB
Vijana, Tunaitwa kuwa Watakatifu!
Maisha ya Kiroho Kwa Vijana – 2
 
Katika makala iliyotangulia tulieleza kuhusu maana ya maisha ya kiroho kwa vijana.  Hapo chini tungependa kueleza vipengele saba vinavyoweza kuwasaidia vijana katika safari yao ya kujikamilisha.  Katika kuandika makala hii nimesaidiwa na Prosper Dionis, ambaye ni kijana mtanzania.  Kwa namna nyingine anaeleza jinsi yeye mwenyewe anavyoishi maisha ya utakatifu.
 
1. Kuadhimisha Maisha kwa Furaha
 
Kuadhimisha maisha kwa furaha ni ile hali ya kutambua ubora wa maisha na kutoruhusu mahangaiko ya maisha kutukatisha tamaa.  Maisha ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu.  Zawadi hii ni kwa ajili ya kulindwa, kukuzwa na kuadhimishwa.  Taabu za maisha wala mahangaiko ya kila siku hayapaswi kuwa vizuizi vya sisi kutofurahia maisha. Kuadhimisha maisha kwa furaha ni fikra niliyo nayo kwamba maisha ni zaidi ya magumu ninayokutana nayo kwa sasa.  Kuadhimisha maisha ni kupokea zawadi ya maisha kama yalivyo, pamoja na taabu na […]

Continue reading


Lectio Divina

UTUME KWA VIJANA 12
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Lectio Divina Kwa Vijana
 
Tangu mwaka 1985, imekuwa desturi katika Kanisa Katoliki kuadhimisha Jumapili ya Matawi kuwa Siku ya Vijana Duniani. Aidha, kila mwaka katika adhimisho hili Baba Mtakatifu huwa anatoa ujumbe maalumu kwa ajili ya vijana duniani kote.  Hata mwaka huu wa 2006, katika adhimisho la 21 la Siku ya Vijana Duniani (9 April 2006), Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kwa vijana wote: “Dhamira ninayopendekeza kwenu ni kutoka Zaburi 119: 105 –  “Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.”
 
Katika ujumbe wake anasisitizia kuwa vijana wa siku hizi tunaishi katika mazingira magumu yenye falsafa za uongo na maadili potofu.  Katika mazingira haya ya giza Neno la Mungu ndilo linaloweza kuiangaza njia yetu.
 
Papa anatukumbushia maneno ya mwandishi wa Waraka kwa Waebrania anayesema: “Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo […]

Continue reading


Vijana na Tabia hatari

UTUME KWA VIJANA 13
Sahaya G. Selvam, SDB

Sababu za Vijana Kujingiza katika Tabia za Hatari
na Namna ya Kuwasaidia
 
Katika makala hii tunashirikisha namna ya kuwasaidia vijana ili waweze kuvuka vikwazo vinavyoweza kuwafanya wasifikie malengo waliojiwekea maishani mwao. Tunatambua kwamba, yapo mambo mengi yanayoweza kuwachelewesha au kuwakwaza vijana kutofikia malengo yao ya maisha. Baadhi yake ni kama:

Dawa za kulevya
Ulevi
VVU/Ukimwi
Mimba kabla ya wakati,  n.k.

 
Katika makala hii, tunaelezea sababu chache zinazopelekea vijana (wasichana) kupata mimba kabla ya wakati. Pia tunapendekeza namna ya kuweza kuwasaidia ili wasijikute katika mtego huu na pia waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Ingawa sababu hizi zinawalenga wasichana moja kwa moja, hata hivyo zinaweza kutumika kwa wavulana pia, kwa vile wavulana wanajiingiza katika mambo haya kirahisi kuliko wasichana.
 
Bi. Tricia M. Davis amefanya utafiti kati ya wasichana wapatao 500 wenye umri wa miaka chini ya 19, waliowahi kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika utafiti wake anaeleza sababu saba […]

Continue reading


Spoti na Utume kwa Vijana

UTUME KWA VIJANA 14
Sahaya G. Selvam, SDB

Spoti na Utume kwa Vijana
 
Ujana ni kipindi katika maisha ya binadamu chenye nguvu nyingi.  Spoti ni mkondo mzuri wa kutumia nguvu hii, na pia njia nzuri ya kujiburudisha kwa vijana.  Burudani ina sehemu yake muhimu katika maisha ya binadamu ili tuwe na afya ya kimwili na ya kiakili.  Ndiyo maana binadamu anaitwa homo ludens, yaani, binadamu mchezaji!  Anapotumia nguvu yake kwa ajili ya kutafuta riziki, hii ni kazi; lakini anapofanya mambo ya burudani na ubunifu bila kutafuta faida yoyote, huu ni mchezo.
 
Basi, katika makala hii ningependa kushirikisha nanyi mawazo machache kuhusu spoti na utume kwa vijana.  Yaani, jinsi michezo, hasa spoti, inaweza kutumika vizuri katika malezi ya vijana. (Michezo kwa ujumla inaweza kumaanisha hata ngoma na tamthilia, lakini spoti ni michezo inayofanyika uwanjani na kuwapa watu nafasi ya kukimbia na kuvinyosha viungo vya mwili.)  Michezo ni njia nzuri ya kuwavutia vijana katika mazingira […]

Continue reading