Familia na Vijana

UTUME KWA VIJANA 5
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Kuwawezesha Vijana Kujenga Familia za Kikristu
 
“Kizazi hiki kimepotea. Vijana wa siku hizi hawana msimamo.  Kuna mmomonyoko wa maadili….” Haya ndiyo malalamiko tunayosikia kutoka kwa watu wazima.  Ukweli ni kwamba, tuwaleavyo vijana ndivyo wakuavyo! Hali ya vijana wa siku hizi ni matokeo ya hali ya familia zetu.  Na hali ya familia zetu si ya kujivunia.
 
Padre Shorter, mtaalamu wa mambo ya kijamii na kitamaduni, analalamika, “Katika jamii za Afrika siku hizi, mfumo wa familia umeathiriwa na mabadiliko ya kijamii na kimila.  Taratibu za jando na unyago zimeanza kupotea. Malezi kuhusu maisha ya kifamilia hayatolewi nyumbani wala shuleni.  Hivyo, vijana wamepoteza msimamo wao, nao kujiingiza katika mapenzi ovyo.” (African Culture: An Overview, 1998, p.95)
 
Mimi naamini kwamba ili kugeuza hali ya familia zetu kuna njia moja tu: inatubidi tuanze na vijana wetu.  Ingawa wengi wao wanatokea familia zilizobomoka, wanaweza kuzuia hali hii isiendelee zaidi.  Wanahitaji kuwezeshwa kuamua […]

Continue reading


Vyama vya Vijana – 1

UTUME KWA VIJANA 6
Sahaya G. Selvam, SDB

Vyama Mbalimbali na Malezi ya Vijana
 
Kuwapenda watu, na kupendwa na watu ni mojawapo ya mahitaji ya kila binadamu. Hitaji hili linaamshwa wakati wa ujana. Hali hii hutokana na mabadiliko ya kimaumbile, kihisia na ya kiakili yanayotokea wakati wa ujana.  Ndiyo maana vijana huwa wanahangaika sana na suala la kutafuta marafiki na namna ya kukuza mahusiano na watu, hasa uhusiano na watu wa jinsia tofauti.
 
Malezi ya jumla kwa vijana yanapaswa kuwapa vijana nafasi ya kukomaa kihisia na kijamii. Ukomavu huu unaweza kukamilishwa kwa njia ya vikundi na vyama vya vijana. Hakuna anayeweza kujifunza namna ya kujenga mahusiano yanayofaa isipokuwa kwa njia ya kupata nafasi ya kuwa katika mazingira ya kuzoeana na watu.  Kazi ya vyama vya vijana ni kuwatengenezea vijana mazingira haya.  Vijana wenyewe wanapenda sana kujiunga na vikundi mbalimbali na kushiriki katika shughuli za vikundi kwa sababu ya hitaji lao la kupenda na […]

Continue reading


Vyama vya Vijana -2

UTUME KWA VIJANA 7
Sahaya G. Selvam, SDB

Mambo Yatiayo Chachu katika Vyama vya Vijana

 
Katika makala iliyopita nilieleza kuhusu umuhimu wa vyama katika malezi ya vijana, niliorodhesha pia aina za vyama pamoja aina mbalimbali za shughuli zinazoweza kufanyika katika vikundi vya vijana.  Katika makala hii ningependa kutaja na kueleza vipengele vichache vinavyosaidia kufanikisha vyama vya vijana.
 
 
1. Mfumo na Uongozi
 
Endapo chama cha vijana kitafanikiwa kutolea malezi ya jumla kwa vijana ni lazima kiwe mfumo mzuri, pamoja na uongozi bora. Ingawa mfumo wa chama unaweza kuwa tofauti kadiri ya malengo yake, hapa tunaweza kutaja mfumo wa jumla ambao unafaa kwa chama chochote kile.  Kila chama kina wanachama wake, na viongozi wake ambao wanachaguliwa au kuteuliwa na wanachama. Uongozi unaweza kuundwa na watu kama watatu au watano kadiri ya mahitaji ya chama. Kuwa na watu wengi katika uongozi hakusaidii sana.   Aidha, kila chama cha vijana lazima kiwe na mlezi, walau mmoja,  […]

Continue reading


Vijana na Vyombo vya Mawasiliano

UTUME KWA VIJANA 8
Sahaya G. Selvam, SDB
Vijana na Vyombo vya Mawasiliano

Tupende tusipende nyakati hizi za karne ya 21 tumelazimika kutumia vyombo mbalimbali vya mawasiliano, kama vile, magazeti, simu, redio, kinasa sauti, runinga, video, mtandao, n.k. Vyombo hivi vimechangia katika kufanyia dunia yetu kuwa ndogo sana.  Vinachangia katika kuendeleza utandawazi, na katika usambazaji wa utamaduni wa kimagharibi.  Tunaweza kuvitumia vyombo hivi kwa ajili ya kujielimisha na kujiburudisha.  Maendeleo ya vyombo hivi yanatubabaisha.  Yaani, kila wakati vyombo hivi vinakuwa vya teknolojia mpya na vya rahisi kutumia.
 
Kwa vile, ni kawaida kwa vijana kuvutiwa na mambo mapya, hata maendeleo ya vyombo vya mawasiliano yanawashangaza sana. Vijana wanapenda pia kuunganika daima na vijana wenzao kwa njia ya kuvitumia vyombo hivi.  Kwa hiyo, wao huwa wanapenda kuzitumia aina mpya za vyombo vya mawasiliano, na pia kuvitumia sana.
 
Dunia ya mawasiliano inaweza kuchochea ubunifu wa vijana. Inaweza kuwasaidia kujielimisha na kujiburudisha. Aidha, inaweza kusababisha vijana kupoteza mali na […]

Continue reading


Siku ya Vijana Duniani

UTUME KWA VIJANA 9
Sahaya G. Selvam, SDB
 
“Tumekuja Kumwabudu”
Siku ya Vijana Duniani na Utume Kwa Vijana
 
Tarehe 16 hadi 21, mwezi Agosti, mwaka 2005 vijana wapatao millioni moja wanatarajiwa kukutanika huko Koloni nchini Ujerumani.  Kongamano hili limekuwa maarufu sana na linajulikana kwa jina la “Siku ya Vijana Duniani” – World Youth Day.  Siku ya Vijana Duniani (SVD) huadhimishwa kila mwaka katika majimbo ya Kanisa Katoliki siku ya Jumapili ya Matawi.   Lakini mara kwa mara huadhimishwa kimataifa, kwa muda wa wiki moja, kama hii ya mwaka huu huko Koloni. Kwa kawaida, kabla ya wiki ya kongamano lenyewe vijana hukaribishwa katika majimbo mbalimbali ya nchi husika. Wiki kabla ya SVD katika majimbo inawapa vijana wageni nafasi ya kushiriki katika maisha ya vijana wenyeji, na kubadilishana mawazo kuhusu matatizo ya dunia na hali ya Kanisa.  Wiki ya “World Youth Day” yenyewe ina vipindi vya Katekesi, nafasi za sala, na hija; wiki ya kongamano hufungwa kwa […]

Continue reading